Tafsiri ya Ndoto: kujirudia kusoma shule ya msingi

kujirudia kusoma shule ya msingi Imepokelewa na Siri za Ndoto tarehe 2025-11-16 11:38:27 🌙 Maelezo ya Ndoto: “kuna ndoto Moja ambayo imekuw...

kujirudia kusoma shule ya msingi

Imepokelewa na Siri za Ndoto tarehe 2025-11-16 11:38:27

🌙 Maelezo ya Ndoto:

“kuna ndoto Moja ambayo imekuwa ikijirudia mara kwa mara yaani naota kuwa nasoma tena nikiwa shule ya msingi kabisa ikiwa nmemaliza masomo yangu ya shule ya msingi mwaka 2014 lakini Leo hii Bado naota nikiwa nasoma shule ya msingi,hapo nashindwa kuelewa shida ni nini”

✨ Tafsiri na Ufafanuzi wa Kiroho

👨‍🏫 Mfasiri: Mfasiri wa Ndoto
Maelezo Ya Mwanzo..
Mwanzo 40:8
"[8]Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. "

Hakika Mungu Ndiye Atafsiriye Ndoto.. ?

Maana Ya Ndoto
Amen Amen Hakika Mungu Husema Na Sisi Kwa Ndoto.

Yesu anakusemesha kuhusu hari yako Ya kiroho. Licha Yakuwa umekwisha kumaliza masomo yako Ya Msingi 2014 Na mengine lakini unapewa taarifa kuwa level yako ya Elimu yako ya kiroho bado ipo chini Na unahutaji kurudi na kujifunza upya.


Nini chakufanya
1: Roho Mtakatifu ndio Mwalimu wetu. Unahitaji kumkaribisha Roho Mtakatifu aweze kuwa Mwalimu wako akufundishe Na kukujuza unayo paswa kuyafanya kujifunza.
Yohana 14:26
[26]Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

2: Unahitaji Kuwa unahuzuri Mikusanyiko ya Ibada Na Sala Na mikutano ili uzidi kujifunza Na kulisikiliza Neno la Mungu.

3: Waweza kumuona Mtumishi Wa Mungu aliye Karibu Yako au wasiliniana nasi Tuweze kukuunganisha Na Madalasa ya Wokovu uweze kujifunza zaidi Amen

Namba: 0710105909


Mithali 4:13-19
[13]Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
Mshike, maana yeye ni uzima wako.
[14]Usiingie katika njia ya waovu,
Wala usitembee katika njia ya wabaya.
[15]Jiepushe nayo, usipite karibu nayo,
Igeukie mbali, ukaende zako.
[16]Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara;
Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
[17]Maana wao hula mkate wa uovu,
Nao hunywa divai ya jeuri.
[18]Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo,
Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
[19]Njia ya waovu ni kama giza;
Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
📖 Mithali 4:13-19
“Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo. Even in laughter the heart is sorrowful; and the end of that mirth is heaviness. [14]Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake. The backslider in heart shall be filled with his own ways: and a good man shall be satisfied from himself. [15]Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. The simple believeth every word: but the prudent man looketh well to his going. [16]Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai. A wise man feareth, and departeth from evil: but the fool rageth, and is confident. [17]Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. He that is soon angry dealeth foolishly: and a man of wicked devices is hated. [18]Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa. The simple inherit folly: but the prudent are crowned with knowledge. [19]Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki. The evil bow before the good; and the wicked at the gates of the righteous.”

Imetolewa na Siri za Ndoto App — Pata tafsiri za ndoto zako kulingana na Maandiko Matakatifu.

COMMENTS

Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content